Professor Jay Nikusaidiaje Download Mp3
Professor Jay Nikusaidiaje Mp3 Download. With assist from Ferooz, Professor Jay has delivered to us a production that hits right in the feels via Nikusaidiaje.
Lyrics
Umesahau ulipotoka hujui unapokwenda
Ukapata kiburi kuona mi nakupenda Nilikuthamini na letu penzi kulienzi Na leo siamini kama umenisaliti mpenziKumbuka nilikukuta kijijini sigimbi
Umebeba mahindi na furushi la magimbi Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitajiKigoli mwenye umbo kama la mdori
Wala sikutaraji ungepiga nami stori Nilifurahi kuweza kukufahamu Na nikakuahidi subiri zangu salamuKwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi
Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumbaWakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa
Niliapa kujua iwapo ningekukosa Walinikabidhi nirudi nawe mjini Na nikakusisitiza mjini kuwa makiniNafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandamaKuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulanaAlikuwa mzuri mithiri ya malaika
Alipotua mjini Zubeda ni patashika Hakika alionekana alikuwa mgeni wa jiji NIlipovua viatu nilivikuta ndani ya frijiAlifanya vibwenga washikaji wakanicheka
Hakutaka kitanda alilala kwenye mkeka Alipokuwa akiona magari alikimbia Akimuona mtu kwenye TV anamuamkiaKila alichofanya alikuwa anakosea
Nilimvumilia kwa kuwa hajazoea Hakai kwenye sofa alikuwa anakaa chini Mafuta ya kupikia eti anayapaka mwiliniNamnunulia soda hataki anataka togwa
Nikimletea keki hataki anataka boga Majirani walimpenda sababu ya uzuri wake Nasikitika mashangingi wakawa rafiki zakeAkaanza kunywa pombe alipokwenda kusuka
Usiku anatoroka tena kwa kuruka ukuta Nilipokuwa natoka, nae nyuma antoka Nikimtuma kitu anadai eti amechokaNikienda kazini ndani analeta mabwana
Magari ya kifahari yakawa yanapishana Hakika starehe za dunia zikamtenda Na hatimaye hata nyumbani pia akatowekaNafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandamaKuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulanaNilipigwa na butwaa, mtaani walinishangaa
Nilikosa raha hata nafsi ilikata tamaa Sikujua huyu binti ni mzima au amekufa Ilibidi niombe watu msaada wa kumtafutaKumbe anaonekana viwanja vya kila aina
Leo yuko na mzungu na kesho yupo na mchina Nilipata shahuku ya kutaka japo kumuona Ingiwa niliamini moyoni ingenichomaKweli tulimtafuta kwenye kumbi tofauti
Ili nihakikishe kweli hajapatwa na mauti Nikamkuta casino la wadachi na walatino Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyoPechiechipinyo na pamba za mandarino
Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo Hakika alipendeza kwa staili alizocheza Na kila aliyemtazama alitamani kumchombezaKwa pozi na dharau alijifanya amenisahau
Akaniona takataka mbele ya washikadau Ilibidi niondoke machozi yakinilenga Shetani kashanitega na tunda langu kamegaAkapata mimba aliyempa hakumtambua
Na wote aliowafata eti wakakana kumjua Zubeda na mimba yake hakuwa na pakuishi Hakujua ale nini na vipi apate ridhikiGhafla hifadhi yake ikawa ni stendi ya basi
Siku nyingine mvua ilimnyeshea kupita kiasi Akarudi nyumbani eti arudiane nami Kurudi kwao hataki, mi na familia ndaniNafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi
Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandamaKuwa nawe haitawezekana mpenzi
Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulanaListen online and The Lyrics, Video of your favorite Music.
Stream, Listen and Download Below.
Mp3 Music Download: Professor Jay – Nikusaidiaje Ft Ferooz